Laina Finance

Terms of Service

Last Updated: 28 August 2022

Vigezo na Masharti ya matumizi ya huduma za Laina Finance Limited.


Vigezo na Masharti haya ('Masharti ya Matumizi ') vinanapatikana kwa Watumiaji wa Huduma ya Laina Finance na vitahusika mara moja unapojiunga na kupata huduma ya Laina Finance au kupitia USSD *150*47# ('Huduma').

Ieleweke ya kwamba Huduma za mikopo zinazotolewa na Laina Finance kupitia makampuni washirika pia na kupitia USSD *150*47# kwa wateja wote (watumishi wa serikali Pamoja na wateja wasio watumishi wa serikali). Huduma hii inatolewa pia kwa wateja wenye kutumia mitandao ya simu kama vile Vodacom pamoja na M-Pesa, Airtel Money Pamoja na Tigopesa ambao wanaopatikana katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuzingatia Masharti ya Matumizi haya.
Laina Finance Limited mara kwa mara itahakiki nyaraka zako za utambulisho au kurekebisha Masharti ya Matumizi haya au kutathmini/kupitia upya kiwango chako cha mkopo. Pia Laina Finance ina haki ya kukubali au kukataa ombi lako la mkopo.


KUKUBALI VIGEZO NA MASHARTI.

Kabla ya kuingia au kujiunga na huduma hii, unapaswa kusoma kwa uangalifu na kuelewa masharti haya ya matumizi yanayosimamia upatikanaji wa matumizi na uendeshaji wa Huduma. Kama hukubaliani na vigezo na masharti haya, tafadhali bonyeze “Sitisha” kwenye huduma ya kujiunga kupitia USSD.Itambulike ya kwamba


1.1. . Huduma zinazopatikana katika USSD ya Laina *150*47# ni Pamoja na kuangalia kiwango cha mkopo, kufanya marejesho, kuangalia mpango wa marejesho ya mkopo, kuangalia salio la deni n.k. Mikopo yote hutolewa kwa kupitia vyanzo au njia za mauzo (sales channels) za kampuni washirika au maduka ya kampuni zinazoshirikiana na Laina Finance ikiwemo maduka yote ya Vodacom Tanzania, Maduka ya Samsung kote nchini, Maduka na mawakala wa Vivo kote nchini n.k.


1.2. Kwa kutumia huduma hii, utakuwa umeisoma, umeelewa na kukubaliana na vigezo na Masharti ya Matumizi: Kwa kubonyeza chaguo 'Kukubali' wakati wa kujiunga pale inapokuomba uhakikishe kuwa umesoma, umeelewa na umekubali kutekeleza vigezo na masharti haya na utakuwa umekubali masharti ya matumizi pia kwa kutumia au kuendelea kutumia na huduma ya Laina Finance Limited.


1.3. Kwa kujiandikisha kwa Huduma hii, unakubali kuzingatia na kufuata masharti ya matumizi haya kama yatakavyokuwa yanafanyiwa marejeo na kurekebishwa mara kwa mara na unathibitisha kuwa vigezo na masharti hayaathiri haki nyingine yoyote ambayo tunaweza kuwa nayo kisheria au vinginevyo kuhusu usajili wako, upatikanaji na matumizi ya huduma.



ADA ZA MKOPO.

1 Riba ya asilimia tatu nukta tano (3.5%) kwa mwezi ya kiasi cha mkopo kilichobaki (Yaani reducing balance). Hii ni wastani wa asilimia 24% kwa mwaka (Yaani annual effective interest Rate)

2 Ada ya kuandaa mkopo ina vipengele vifuatavyo -
A. Ada ya utayarishaji mkopo ni asilimia tatu (3%) ya bei halisi kifaa/simu ya sokoni.
B. Ada ya kinga (Indemnity) ni asilimia sita (6%) ya bei ya kifaa/simu sokoni.
C. Ada ya kukusanya deni ni asilimia tano (5%) ya bei ya kifaa/simu ya sokoni.
Jumla ya Ada ya mkopo itakuwa ni asilimia kumi na nne (14%) tu kwa mkopo wote kabla ya kodi na makato ya serikali.

3. Mteja atapaswa kulipia gharama za kuandaa mkopo zilizoainishwa pamoja na kodi za serikali. Ada zote zitajumlishwa kwenye kiwango cha mkopo na zitalipwa wakati wa kufanya rejesho au malipo ya awali.

4. Viwango vya Mkopo Pamoja na vigezo na masharti vinaweza kupitiwa na kubadilishwa mara kwa mara na tunahaki ya kupitia tena na kutofautisha viwango vya Mkopo kwa taarifa au bila kutoa taarifa; ingawa (siyo wajibu wetu) tutajaribu kukupa taarifa kuhusu utofauti wowote wa viwango vya Mkopo pale itakapobidi.

5. Kwa kujiunga na huduma za Laina Finance kupitia USSD namba *150*47# na kukubali vigezo na masharti vinavyopatikana kwenye mkataba uliosaini wakati wa kuchukua mkopo, mteja unaridhia na kuthibitisha kuwa umesoma, umeelewa, umekubali na kuridhia vigezo vyote na masharti Pamoja na ada zilizoainishwa. Aidha umeridhia kwa Laina Finance (Laina) kama ifuatavyo:-
5.1 Kwa Watumishi wa serikali ambao wamekuwa wateja wa Laina na pia kwa kutumia huduma zetu kupitia USSD yetu, unaridhia na kumpa ruhusa (kumwelekeza) Mwajiri wako kwamba wakati wowote ule endapo kutatokea mabadiliko ya Mwajiri kabla ya kuisha kwa mkopo ambao umechukua Laina Finance, kuheshimu na kutekeleza makubaliano au madai yatakayoletwa na Laina hadi pale mkopo wote utakapokuwa umekwisha.
5.2 Kwa kiwango cha mkopo ulichopata, unapaswa kulipa chote ndani ya muda uliochagua, bila kuchelewesha tangu tarehe ambapo umepata mkopo(tarahe ya kwanza ya kupata mkopo). Hutaweza Kupata mkopo mpya au kuongeza nyingine ikiwa una deni la awali au umekiuka masharti na matumizi ya Laina Finance Ltd.
5.3 Taarifa zangu za mkopo na mwenendo wa marejesho kuangaliwa na kuwasilishwa kwenye taasisi za kutunza kumbukumbu ya mkopo (Credit Reference Bureau) kama sehemu ya utaratibu pendekezwa wa kisheria. Pia ninaridhia ya kwamba taarifa zangu za ulipaji wa mikopo ya nyuma kuangaliwa katika taasisi yoyote ya kutunza kumbukumbu ya mkopo (CRB) endapo Laina itakuwa na nia ya kujiridhisha na sifa za ulipaji wangu wa mikopo mingine.
5.4 Endapo mteja hatolipa kwa wakati au kuchelewesha kufanya marejesho ya mkopo kutokana na sababu yoyote ile basi ninaidhinisha na kutoa ridhaa kwa Laina kutoza ada ya asilimia sifuri nukta tano (0.5%) ya rejesho liliyobaki kama adhabu ya kucheleweshwa kwa kila siku moja ya ucheleweshaji.
5.5 Kuibiwa, kuharibika au kupotea kwa simu/kifaa/bidhaa haitakuondolea wala kukupunguzia wajibu wa kumalizia marejesho ya mkopo na ada zote endapo kutakuwa na ucheleweshaji.
5.6 Endapo kifaa/simu imeleta hitilafu au tatizo la kiufundi ndani ya muda wa waranti, mteja anatakiwa kuirudisha dukani ili ifanyiwe marekebisho kulingana na waranti ya simu hiyo. Aidha, Laina haiusiki na suala hili hivyo haitahusishwa na haitawajibishwa kwa namna yoyote ile.
5.7 Ninaielekeza na kuipa ruhusa na kuridhia kwa kampuni husika ya mitandao ya simu (Vodacom/Tigo/Airtel/TTCL/Zantel) kuweza kutoa taarifa za namba zangu nyingine zilizosajiliwa na kitambulisho changu cha NIDA endapo kampuni ya simu itapewa taarifa rasmi kutoka Laina juu ya changamoto za upatikanaji wangu na kuchelewesha au kutokufanya marejesho yangu ya mkopo ndani ya wakati au kwasababu yoyote ile itakayotolewa inayopelekea mimi kushindwa kutimiza wajibu wangu wa kulipa mkopo.
5.8 Laina ina haki na uhuru wa kunikumbusha juu ya marejesho yangu ya mkopo wa malipo ya simu/kifaa muda wowote wakati wa mkataba huu ukiwa hai kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi yaani sms au kunipigia kwenye namba iliyotajwa hapo juu au kunipigia kwa namba yoyote ambayo imesajiliwa kwa kitambulisho changu cha NIDA. Pia Laina inahaki ya kukutumia ujumbe unaohusiana na huduma nyingine zinazotolewa na Laina Pamoja na washirika wake wapya.
5.9 Laina ina haki ya kufanya mabadiliko ya vigezo na masharti bila kutoa taarifa kwa mteja ili mradi mabadiliko hayo yanapatikana kupitia ukurasa wa tovuti ya www.lainafinance.co.tz.
5.10 Endapo mteja atashindwa kukamilisha marejesho kwa utaratibu tuliokubaliana kwa namna moja au nyingine, basi mteja anatoa ridhaa kwa Laina kutumia njia mbadala ili kuhakikisha deni lote linalipwa. Aidha, njia mbadala ambazo ninaridhia zitumike ni pamoja na njia zifuatazo.
5.10 (a) kukatwa moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yangu ya simu ya mtandao wowote ule iliyosajiliwa kwa majina ya yangu na kitambulisho cha NIDA kilichotajwa hapo juu.
5.10 (b) Kukatwa fedha sawa na kiwango cha deni lililobaki kutoka kwenye akaunti yangu ya benki iliyofunguliwa kwa majina yangu bila taarifa yoyote ile kuja kwangu.
5.10 (c) Ninaridhia kulipa gharama zote na ada zitakazotozwa kutokana na usumbufu wowote nitakaokuwa nimesababisha.
Pia vigezo na masharti haya kutumika kutoa mwongozo wa makubaliano na wajibu wa Laina na mteja juu ya huduma hii ya mkopo wa malipo ya bidhaa/simu na kuanza kutumika tangu tarehe ya kuingia makubaliano.

6 Iwapo una malalamiko yoyote, maswali au mapendekezo yoyote kuhusiana na mkopo wako kwa njia ya simu tafadhali piga 0222774012 katika simu yako ya mkononi ili uwasiliane na Kituo cha Huduma kwa Wateja.



7. MUDA WA MALIPO.

Muda wa mkopo ni kuanzia miezi Mitatu (3) kwa kima cha chini hadi hadi miezi 12 kwa kima cha juu. Aidha, muda huu unatagemea ni mkopo kwa watumishi wa aina gani. Kwa watumishi wa kampuni Binafsi, muda wa marejesho ni hadi miezi sita (6) ila kwa watumishi wa serikali ni kati ya miezi sita(6) hadi miezi mumi na mbili (12) kutegemea na chaguo la mteja.


8. TAARIFA ZAKO BINAFSI.

Kwa vile sheria inaruhusu, kwa kuomba mkopo, unatoa idhini kwa Laina Finance ya kukusanya na kutumia Taarifa zako Binafsi kama zilivyoelezwa hapo chini.
8.1 Ni taarifa zipi tunazokusanya na kwa nini. Unapoomba mkopo, unakubali kwamba tunaweza kukusanya baadhi ya taarifa kuhusu wewe kutoka kwenye mtandao unaotumia kwa kutumia namba yako ya simu utakayotumia Pamoja na namba yako ya kuajiriwa kwa watumishi wa serikali ili kufanya tathmini ya kiasi cha mkopo (“Kiasi cha Mkopo”). Hii inajumuisha namba yako ya simu ya mkononi, majina yako, tarehe ya kuzaliwa, namba ya kitambulisho cha taifa au pasipoti na taarifa zote kuhusu Akaunti yako ya mtandao wa simu utakayotumia kwa usajili.
8.2 Ukusanyaji wa Taarifa zako Binafsi ni wa kisheria (lazima). Hii ina maana kuwa ili upatiwe mkopo kutoka kwetu, unahitaji kukubali kuchangia Taarifa zako Binafsi nasi, Mtoaji na baadhi ya pande nyingine.
8.3 Iwapo hatutapokea Taarifa zako Binafsi, hatutaweza kukupatia mkopo. Hii ndio sababu ni lazima ukukubali kuturuhusu kupata Taarifa zako Binafsi.
8.4 Kwa vile sheria inaruhusu, kwa kukubali Masharti haya ya huduma hii, unatoa idhini na kumruhusu Laina Finance kuchangia Taarifa zako Binafsi na :
8.4.1 Mamlaka yoyote ya ndani au ya kimataifa ya utekelezaji wa sheria au mamlaka ya usimamizi inayohusika au wakala wa serikali kusaidia kuzuia, kugundua au kuchunguza matukio ya uhalifu au udanganyifu.
8.4.2 Upande mwingine wowote ulioudhinishwa chini ya sheria zilizopo na Shirika lolote la Kumbukumbu za Mikopo ili (pamoja na mambo mengine) kuendesha uchunguzi wa mikopo au kutoa taarifa kwaShirika la Kumbukumbu za Mikopo kama itakavyokuwa imeelekezwa au kutakiwa kisheria.Tutakuwa na Taarifa zako Binafsi kwa kadri itakavyohitajiwa wakati tukiendelea kukupatia huduma zetu na tukiendelea kukupatia mikopo zaidi.
8.4.3 Unaweza kuona taarifa Mtoaji alizonazo kuhusu wewe na kuomba kurekebisha taarifa zisizo sahihi. Hii inaweza kuwa gharama inayofaa iliyojumuishwa katika kutekeleza haki hii inayoweza kubadilika.
8.4.4 Una haki ya kutuomba tufute Taarifa zako Binafsi zote, hata hivyo baada ya hapo hatutakupatia mikopo yoyote zaidi.
8.4.5 Tunakuahidi kwamba tutafuata ulinzi wa kiusalama wa kutosha na mkubwa ili kulinda matumizi yoyote yasiyoruhusiwa au kupata Taarifa zako Binafsi.