Last Updated: 10 February 2024
Laina Finance Limited (Ambayo itatambulika kama
“Laina”)
KUKUBALI OMBI LAKO LA KUUZIWA SIMU (MODEL) KWA NJIA YA UWEZESHAJI UNAOFUATA UTARATIBU WA MKATABA WA MURABAHA
Tunarejea maombi yako yaliyotolewa tarehe…. Mwezi…..202.. yaliohusu kuuziwa simu (Model) kwa njia ya uwezeshaji (financing) kwa kufuata utaratibu wa mkataba wa Murabaha. Tunafurahi kukutaarifu kuwa LAINA FINANCE LIMITED (hapa inajulikana kama "Muuzaji") imeridhia kukuuzia simu tajwa hapo juu kwa kufuata utaratibu wa mkataba wa Murabaha kwa makubaliano yafuatayo;
1. GHARAMA NA FAIDA
1.1 Muuzaji atakuuzia simu (Model and Specification) kwa Tsh. mfano, (120,000) (Shilingi za Tanzania Laki moja na elfu ishirini tu) ambayo inagawanyika kama ifuatavyo; gharama ya simu (Model) ni Tsh. (100,000) (Shilingi za Tanzania Laki Moja tu) na faida ya Tsh. (20,000) (Shilingi za Tanzania Elfu Ishirini tu).
2 MUDA WA UWEZESHAJI
2.1 Uwezeshaji huu utaendeshwa kwa kipindi cha miezi sita/ kumi na miwili kwa mikupuo sawa ya malipo ya Tsh. mfano,(10,000) (Shilingi za Tanzania Elfu kumi tu) kila mwezi
3 DHAMANA YA UWEZESHAJI
3.1 Uwezeshaji huu utadhaminiwa na simu (Model and specification) ambayo utauziwa mpaka pale utakapomaliza kufanya malipo yote kama yalivoainishwa hapo juu.
4 MASHARTI YA JUMLA
Kwa kuchagua na kujiunga kutumia huduma hii inayotolewa na LAINA FINANCE LIMITED, mteja anaridhia na kukubaliana na vigezo na masharti yafuatayo;
4.1 Endapo mteja ni muajiriwa wa serikali au Sekta binafsi anaridhia kumuelekeza na kumpa ruhusa Mwajiri wake kupokea maelekezo kutoka LAINA FINANCE LIMITED ya kukata kutoka katika mshahara wake kiwango sawa na malipo ya kila mwezi yaliyotajwa katika sehemu 2.1 ya makubaliano haya na kuweka katika Account ya LAINA FINANCE LIMITED iliyoelekezwa na LAINA FINANCE LIMITED yenyewe kama malipo ya mauziano haya hadi pale malipo yote yatakapokuwa yamekamilika.
4.2 Ninaridhia kwamba Namba ya makubaliano ya mauziano (Consent code) kutumika kama saini yangu.
4.3 Kupokea simu kwa mauziano yenye thamani kama ilivyoorodheshwa katika sehem 1.1 ya
4.4 makubaliano haya na ninakubali kuwajibika kulipia manunuzi ya bidhaa husika kulingana na utaratibu wa malipo ulivyoainishwa katika makubaliano haya.
4.5 Taarifa zangu za makubaliano ya mauziano na mwenendo wa malipo ya uwezeshaji (financing) yangu ya nyuma kuangaliwa na kuwasilishwa kwenye taasisi za kutunza kumbukumbu ya mkopo (Credit Reference Bureau) kama sehemu ya utaratibu pendekezwa wa kisheria. Pia ninaridhia ya kwamba taarifa zangu za ulipaji wa mikopo ya nyuma kuangaliwa katika taasisi yoyote ya kutunza kumbukumbu ya mkopo (CRB) endapo LAINA FINANCE LIMITED itakuwa na nia ya kujiridhisha na sifa za ulipaji wangu wa mikopo mingine.
4.6 Endapo sitalipa kwa wakati kwa sababu yoyote ile, ninatoa ridhaa kwa LAINA FINANCE LIMITED kufunga au kuzuia matumizi yote ya bidhaa. Gharam azote zinazohusiana na kufunga na kufungua kifaa (Devices locking and unlocking costs) zitabebwa na mteja.
4.7 Endapo sitalipa kwa wakati au kuchelewesha kufanya malipo kutokana na sababu yoyote ile basi ninaidhinisha na kutoa ridhaa kwa LAINA FINANCE LIMITED kutoza ada ya asilimia sifuri nukta tano (0.5%) ya malipo yangu ya awamu ya kila mwezi yaliyobaki kama adhabu ya kuchelewesha malipo kwa kila siku moja ya ucheleweshaji. Ada hii itatumiwa na LAINA FINANCE LIMITED katika shughuli mbalimbali za kusaidia jamii na si uendeshaji wa biashara.
4.8 Kuibiwa, kuharibika au kupotea kwa bidhaa hii haitaniondolea au kunipunguzia wajibu wangu wa kumalizia/kukamilisha malipo.
4.9 Nakiri kutambua kua endapo bidhaa husika imeleta hitilafu au tatizo la kiufundi ndani ya muda wa siku kumi nan ne (14), nitatakiwa kuirudisha dukani ili ifanyiwe marekebisho kulingana na waranti ya bidhaa hiyo.
4.10 Ninaridhia na kuipa ruhusa kampuni husika ya simu (Vodacom/Tigo/Airtel/TTCL/Zantel) kuweza kutoa taarifa za namba zangu nyingine zilizosajiliwa na kitambulisho changu cha NIDA endapo kampuni ya simu itapewa taarifa rasmi kutoka LAINA FINANCE LIMITED juu ya changamoto za upatikanaji wangu na kuchelewesha au kutokufanya malipo yangu ndani ya wakati au kwa sababu yoyote ile itakayotolewa inayopelekea mimi kushindwa kutimiza wajibu wangu wa kulipa.
4.11 Natoa ridhaa kwa Kampuni ya simu kuikabidhi LAINA FINANCE LIMITED namba za simu zitakazokuwa zinatumika kwenye kifaa/simu chenye IMEI number iliyotajwa kwa lengo la kusaidia kukusanya malipo.
4.12 LAINA FINANCE LIMITED ina haki na uhuru wa kunikumbusha juu ya malipo ya bidhaa niliyochukua muda wowote wakati wa makubaliano haya ukiwa hai kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi yaani sms au kunipigia kwenye namba nilizowasilisha wakati wa maombi au hatua nyingine ya uwezeshaji huu au kunipigia kwa namba yoyote ambayo imesajiliwa kwa kitambulisho changu cha NIDA au kwa namba ya mtu wangu wa karibu niliyemuainisha.
4.13 Kwamba nipo tayari kulipa malipo ya awali (Hamish JIddiyyah) ya uwezeshaji huu kama itakavyoainishwa na muuzaji.
4.14 Endapo mteja atashindwa kukamilisha malipo kwa utaratibu ulioainishwa katika makubaliano haya kwa namna moja au nyingine, basi anaridhia kwa kutoa ruhusa kwa LAINA FINANCE LIMITED kutumia njia mbadala ili kuhakikisha malipo yote yanalipwa. Aidha, njia mbadala ambazo ninaridhia zitumike ni pamoja na njia zifuatazo:-
4.14.1 Kukatwa moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yangu ya simu ya mtandao wowote ule iliyosajiliwa kwa Namba yangu ya kitambulisho cha NIDA kilichoanishwa wakati wa maombi.
4.14.2 Kukatwa fedha sawa na kiwango cha malipo yaliyobaki kutoka kwenye akaunti yangu ya benki iliyofunguliwa kwa majina yangu.
4.14.3 Ninaridhia kulipa gharama zote na ada zitakazotozwa kutokana na usumbufu wowote nitakaokuwa nimesababisha.