Laina Finance

Pata Dawa Terms & Conditions

Last Updated: 10 February 2024

VIGEZO NA MASHARTI YA HUDUMA YA PATA DAWA


1. MASHARTI YA JUMLA YA KUPATA HUDUMA YA PATA DAWA (MANUNUZI NA MAUZIANO)


Huduma ya Pata Dawa inamwezesha Mteja kuweza kukamilisha miamala yake ya manunuzi ya dawa ambayo huenda angeshindwa kukamilishwa kutokana na mteja kutokuwa na kiasi cha kutosha katika akaunti yake ya simu ya mkononi (Yaani tigopesa Account). Mteja anapaswa kujisajili rasmi ili kuweza kupata huduma ya PATA DAWA toka Laina kwa kutumia njia ya kujisajili kama vile, Laina Application, Laina USSD au TigoPesa USSD, tigopesa application au tigopesa whatsapp. Mteja kwa kujisajili, atakuwa amekubaliana na Vigezo na Masharti (Yaani Terms and Conditions) zilizoainishwa hapa na kumuwezesha kupata huduma mbali mbali za Laina kutegemeana na uhitaji wake. Vivo hivyo, Muuzaji atatakiwa kujiunga na huduma ya pata dawa na kukubaliana vigezo na masharti hususani kuchukua wajibu wa kuwa wakala katika kukabidhi dawa kwa mteja wa Laina. Vigezo na masharti haya yatatumika katika kutoa huduma ya PATA DAWA kwa kuzingatia utaratibu wa utoaji huduma za fedha au mikopo inayofuata maadili ya Kiislam (Yaani Islamic Finance – Sharia compliance). Hivyo, vigezo na masharti haya yamegawanyika katika mafungu makuu matatu kama ifuatavyo:-



1. Vigezo na masharti juu ya manunuzi - Duka la Dawa linaiuzia Laina dawa kwa gharama ya Muamala utakaowezeshwa kutumwa. Mara baada ya mauziano haya dawaitakuwa ni mali ya Laina, Laina ataweka faida na kuiuza dawa hiyo kwa mteja.


2. Vigezo na masharti kuhusu Uwakala ---- Muuzaji yaani Duka la Dawa litachukua wajibu wa UWAKALA kutoka Laina kwa madhumuni ya kukabidhi dawa kwa wateja kwa niaba ya Laina kulingana na masharti yaliyowekwa hapa.


3. Vigezo na masharti ya mauziano baina ya Laina na Mteja - Laina itamuuzia mteja Dawa kwa kutumia mkataba wa Murabaha na kuweka faida iliyosawa na asilimia kumi na tatu na nusu yaani 13.5%. Mfano dawa itakayonunuliwa kwa TSh 10,000 kutoka kwa muuzaji au duka la dawa itauzwa kwenda kwa mteja kwa Tsh 13,500.


4. Laina Finance inatoa huduma za fedha chini ya usimamizi wa Benki Kuu Ya Tanzania. Laina Finance inakibali maalumu cha kutoa huduma za fedha zinazofuata maadili ya Kiislam ambayo husimamiwa na kamati maalumu ya Laina Sharia Audit Committee). Hivyo, kwa kutambua haya, Laina Finance inatoa rai kwa wateja wote wa Pata Dawa kuheshimu nia hii na kutumia huduma hii kufanya manunuzi ya bidhaa zinazoendana na maadili ya Kiislamu (Yaani huduma hii isitumike kufanya manunuzi ya bidhaa zisizofuata misingi au maadili ya Kiislam)


5. Katika kutoa huduma hii, Laina imetenga mfuko maalumu (Sharia Fund) ambao utatumika kwaajili ya kufanya shughuli za kijamii na si biashara kufuatana na kanuni sharia kupitia mkataba wa Murabaha.



VIGEZO NA MASHARTI VYA MANUNUZI NA MAUZIANO.



Duka la Dawa lenye taarifa zifuatazo ambaye atatambulika kama “Muuzaji” na kwa pamoja watatambulika kama “Pande” za Mkataba


Jina kamili la Duka la Dawa: ...................................................


Makubaliano ya Mauziano (Sales Contract)


1. MAELEZO YA DAWA NA BEI


1.1. Laina inakubali kununua dawa kutoka kwa Muuzaji kwa gharama itakayoainishwa hapo chini


1.2. Bei ya kila Dawa itaainishwa kipindi cha ufanikishaji wa muamala husika kutegemeana na mahitaji ya mteja. Aidha, Laina imekubali kununua kutoka kwa Muuzaji/Duka la Dawa kwa mujibu wa masharti ya malipo yaliyowekwa hapa chini.

2. MALIPO NA MUDA WA MALIPO

2.1 Kulingana na kiwango cha uwezeshwaji ambacho mteja anastahili kupata kupitia huduma ya pata dawa, Malipo yote yatalipwa kwa kutumia tigopesa kwenda kwa namba ya Lipa Kwa Simu ya muuzaji baada ya kupata uthibitisho wa nia ya kununua kutoka kwa mteja mwenye uhitaji wa kutumia huduma ya pata dawa.


2.2 Laina itafanya manunuzi ya dawa baada ya kupokea uthibitisho wa nia ya kununua kutoka kwa mteja kwa njia ya kielekroniki kupitia huduma ya tigopesa


2.3 Malipo yatafanywa kwa kutumia njia ya malipo iliyoafikiwa kati ya pande mbili za mkataba kama kipengele 2.1 kilivyoainisha.


3. UWASILISHWAJI WA BIDHAA


3.1 Muuzaji atakabidhi bidhaa kwa Laina ndani ya muda maalumu kulingana na makubaliano au maelekezo kutoka kwa Laina.


3.2 Punde tu baada ya kukamilisha malipo, umiliki wa bidhaa au dawa zilizonunuliwa utahamia kwa Laina mpaka muda wa makabidhiano kwenda kwa mteja.


4. HAKI ZA UBORA NA DHAMANA


4.1 Muuzaji/Duka la dawa anahakikisha kwamba Bidhaa zote zinakidhi viwango vya ubora na zinafanya kazi kama ilivyoelezwa.


4.2 Ikiwa Bidhaa itapatikana kuwa na kasoro ndani ya kipindi cha siku (2) tangu tarehe ya kupokea bidhaa, Muuzaji atachukua jukumu la kubadilisha Bidhaa hiyo.


5. MASHARTI YA KUJIONDOA


5.1 Upande mmoja wa mkataba huu hauna haki ya kujiondoa isipokuwa kwa makubaliano ya maandishi kati ya pande zote mbili.


6. MASHARTI MENGINE


6.1 Mkataba huu utaanza kutekelezwa mara moja baada ya Duka la dawa kuridhia namba yake ya Lipa kwa simu iwekwe kwenye huduma ya pata Dawa.


6.2 Pande zote mbili zitaheshimu na kutekeleza masharti yote ya mkataba huu.


6.3 Mkataba huu utasimamiwa na kufuata miongozo ya sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na taratibu za usuluhishi wa migogoro baina ya pande mbili za mkataba huu.


6.4 Naridhia taarifa zangu zinazopatikana kwenye mtandao wa Tigo mfano NIDA,Namba zangu za simu,matumizi yangu ya pes ana majina yangu kmili yaliyotumika katika usajili wa laini zitolewe Kwenda Laina ili kutumika kwa lengo la huduma ya Pata Dawa.


6.5 Mabadiliko yoyote au marekebisho kwa mkataba huu yanapaswa kuwa na maandishi na saini ya pande zote mbili.

6.6 Mkataba huu utadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja ukiwa na hiari ya kujadidi (renew) kwa pande zote mbili.

7. MATUKIO YA DHARURA

7.1 Ikiwa tukio lolote la Matukio ya dharura litatokea, pande zote zitatumia juhudi zao bora kupunguza athari zake na kupata suluhisho la busara kwa mashauriano ya pamoja.

Kwa hivyo, pande zote mbili zinakubaliana na masharti yote ya mkataba huu kama yalivoainishwa hapo juu.



2. VIGEZO NA MASHARTI VYA UWAKALA (Agency Agreement)

Kwa kujiunga na huduma ya Pata Dawa, Duka la Dawa (ambalo ndio ilikua muuzaji katika hatua ya awali) Inakubali wajibu wa kuwa Wakala wa Laina kwa madhumuni ya kumuwezesha WAKALA kukabidhi dawa kwa mteja/wateja kwa niaba ya Laina kulingana na masharti yaliyowekwa hapa.

Jina la Wakala/Duka la Dawa:....................................................

2.1. Duka la dawa linakubali kuwa Wakala wa Muwakilishi wa Laina kwa ajili ya kukabidhi dawa kwa wateja.

2.2. WAKALA anakubali wajibu na kupewa idhini ya kukabidhi dawa kwa wateja baada ya kupata malipo ya manunuzi kukamilika.

2.3. Pande zote mbili zinakubaliana kuweka na kuhifadhi kwa siri taarifa zote za biashara na mawasiliano kati yao.

2.4. Pande zote mbili zinakubaliana kuwa vigezo na masharti haya havitahusisha malipo ya aina yoyote kwa WAKALA kama ada ya utekelezaji wa majukumu yake yaliyobainishwa ndani ya mkataba huu.

2.5. Naridhia taarifa zangu zinazopatikana kwenye mtandao wa Tigo mfano NIDA,Namba zangu za simu,matumizi yangu ya pes ana majina yangu kmili yaliyotumika katika usajili wa laini zitolewe Kwenda Laina ili kutumika kwa lengo la kupata huduma ya Pata Dawa.

2.6. Mkataba huu utaanza pindi Duka la Dawa litakapojiunga katika huduma ya Pata Dawa

2.7. Mkataba huu unaweza kusitishwa na pande yoyote kwa kutoa ilani ya maandishi ya siku thelathini (30) kwa upande mwingine kwa sababu yoyote inayostahiki.

2.8. Kwa lengo la maboresho, Laina inahaki ya kufanya mabadiliko au marekebisho ya mkataba ili mradi mabadiliko hayo yanapatikana katika tovuti ya www.lainafinance.co.tz

2.9. Ilani zote au mawasiliano yanapaswa kutumwa kwa maandishi, barua pepe yaani info@lainafinance.co.tz au kuwasiliana nasi kupitia anuani ifuatayo (Laina Finance Ltd, P.O.Box 77499 DSM) na yanachukuliwa kuwa yamepokelewa wakati wa kufika kwa mawasiliano.

2.11. Ikiwa tukio lolote la Matukio ya dharura litatokea, pande zote zitatumia juhudi zao bora kupunguza athari zake na kupata suluhisho la busara kwa mashauriano ya pamoja.



3. VIGEZO NA MASHARTI YA JUMLA KWA MTEJA

Kwa kuchagua na kujiunga kutumia huduma hii inayotolewa na LAINA FINANCE LIMITED ikishirikiana na Tigo/Zantel, mteja anaridhia na kukubaliana na vigezo na masharti vifuatavyo;

3.1 Mteja akijiunga na kukubali vigezo na masharti kwenye mfumo wa tigopesa kupitia menyu ya Tigopesa mteja atakua amefanikiwa kujiunga na huduma.

3.2 Naridhia taarifa zangu zinazopatikana kwenye mtandao wa Tigo mfano NIDA,Namba zangu za simu,matumizi yangu ya pes ana majina yangu kmili yaliyotumika katika usajili wa laini zitolewe Kwenda Laina ili kutumika kwa lengo la kupata huduma ya Pata Dawa.

3.3 Mteja anaridhia kupokea dawa kwa mauziano yenye thamani kama itakavyoorodheshwa katika jedwali lenye taarifa za manunuzi ya makubaliano haya na anakubali kuwajibika kulipia manunuzi ya dawa husika kulingana na utaratibu wa malipo utakavyoainishwa katika makubaliano haya.

3.4 Mteja anakubali taarifa zake za makubaliano ya mauziano na mwenendo wa malipo ya uwezeshaji (financing) yake ya nyuma kuangaliwa na kuwasilishwa kwenye taasisi za kutunza kumbukumbu ya mkopo (Credit Reference Bureau) kama sehemu ya utaratibu pendekezwa wa kisheria. Pia anaridhia ya kwamba taarifa zake za ulipaji wa mikopo ya nyuma kuangaliwa katika taasisi yoyote ya kutunza kumbukumbu ya mkopo (CRB) endapo LAINA FINANCE LIMITED itakuwa na nia ya kujiridhisha na sifa za ulipaji wake wa mikopo mingine.

3.5 Mteja anaridhia kwamba kuibiwa, kuharibika au kupotea kwa bidhaa/dawa alizonunua kwa mfumo wa pata dawa haitamuondolea au kumpunguzia wajibu wake wa kumalizia/kukamilisha malipo.

3.6 Mteja anakiri kutambua kua endapo bidhaa husika imeleta hitilafu au tatizo ndani ya muda wa siku kumi na nne (14), anatatakiwa kuirudisha dukani ili abadilishiwe kulingana na waranti ya bidhaa hiyo. Aidha atafuata ushauri wa wataalamu mahususi.

3.7 Mteja anaridhia na kuipa ruhusa Tigo Pesa kuweza kutoa taarifa za namba zake nyingine zilizosajiliwa na kitambulisho chake cha NIDA endapo kampuni ya simu itapewa taarifa rasmi kutoka LAINA FINANCE LIMITED juu ya changamoto za upatikanaji wake na kuchelewesha au kutokufanya malipo yake ndani ya wakati au kwa sababu yoyote ile itakayotolewa inayopelekea yeye kushindwa kutimiza wajibu wake wa kulipa.

3.8 Mteja anatoa ridhaa kwa Tigo Pesa kuikabidhi LAINA FINANCE LIMITED namba za simu zitakazokuwa zinatumika kwenye usajili kwa Nida namba yangu kwa lengo la kusaidia kukusanya malipo.

3.9 Mteja anakiri kuwa LAINA FINANCE LIMITED ina haki na uhuru wa kumkumbusha juu ya malipo ya bidhaa aliyochukua muda wowote wakati wa makubaliano haya ukiwa hai kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi yaani sms au kumpigia kwenye namba alizowasilisha wakati wa maombi au hatua nyingine ya uwezeshaji huu au kumpigia kwa namba yoyote ambayo imesajiliwa kwa kitambulisho chake cha NIDA.

3.10 Endapo mteja atashindwa kukamilisha malipo kwa utaratibu ulioainishwa katika makubaliano haya kwa namna moja au nyingine, basi anaridhia kwa kutoa ruhusa kwa LAINA FINANCE LIMITED kutumia njia mbadala ili kuhakikisha malipo yote yanalipwa. Aidha, njia mbadala ambazo anaridhia zitumike ni pamoja na njia zifuatazo:-

4. Kukatwa moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yake ya simu ya mtandao ule iliyosajiliwa kwa Namba yake ya kitambulisho cha NIDA kilichoanishwa wakati wa maombi.

4.1 4.1 Anaridhia kulipa gharama zote na ada zitakazotozwa kutokana na usumbufu wowote atakaokuwa amesababisha.

5. Pale ambapo mojawapo ya upande inashindwa, kwa sehemu au kabisa, kutekeleza majukumu yake hapa kwa sababu yoyote au tukio lisilokuwa la kawaida na linalozidi uwezo wa kudhibiti wa upande husika ("Matukio ya dharura"), kama vile vita (vilivyotangazwa au la), mapinduzi au uasi, tetemeko la ardhi na maafa ya asili, vitendo vya serikali katika uwezo wake wa kifalme, vizuizi au vikwazo, wajibu wa upande huo kutekeleza majukumu hayo yanayoguswa na Matukio ya dharura itasimamishwa kwa kipindi sawa na kucheleweshwa moja kwa moja na kutokea kwa tukio hilo.

5.1 Ikiwa tukio lolote la Matukio ya dharura litatokea, pande zote zitatumia juhudi zao bora kupunguza athari zake na kupata suluhisho la busara kwa mashauriano ya pamoja.

6. Mahali popote ambapo mteja anatakiwa kulipa kiasi chochote kulingana na Nyaraka Kuu kwenye tarehe ya rejesho na hakilipwi ifikapo tarehe hiyo, au kipindi cha nyongeza kilichoruhusiwa na Laina bila kuongezeka kwa bei ya mkataba, mteja hapa anajitolea kulipa faini moja kwa moja kwenye Hazina ya Hisani, iliyoanzishwa na Laina, kiasi kilichohesabiwa kuwa asilimia tano (5%) kila mwaka juu ya faida iliyopangwa kwa kipindi chote cha kuchelewa, ikihesabiwa kwenye jumla ya kiasi kilichocheleweshwa. Hazina ya Hisani itatumika kwa uamuzi kamili wa Laina, kwa madhumuni ya pekee ya vituo vya hisani vilivyoidhinishwa.