1. Laina ni nini?

LAINA ni neno la kifinland likimaanisha Mkopo

2. Laina inafanya kazi gani?

Inampa mteja nafasi ya kununua bidhaa ambayo ameshindwa kuilipia malipo kamili na kuweza kulipa % kadhaa ya ghalama ya bidhaa hiyo wakati laina inaongezea kiasi kilichobaki katika duka ambalo mteja amehitaji kuchukua kifaa, mteja anapewa nafasi ya kulipa kiasi kilichobaki kwa muda wa miezi 3-6-12.

3. Nani ni mteja wa Laina?

Wateja wa Laina ni watu binafsi na makampuni mbalimbali yenye historia nzuri ya kukopa na kufanya marejesho.

4. Ni nini ambacho Laina inakopesha?

Laina inakopesha kifaa mbalimbali vya umeme kama simu, Laptops, Mashine za POS na bidhaa zingine mbalimbali au mkopo wa kibiashara kwa wateja Fulani.

5. Inachukua muda gani kukamilisha usajiri wa mkopo wa Laina?

Katika uhakiki na ukaguzi wa taarifa za mteja, inachukua muda wa sekunde 60 mteja kutambua amefuzu kupata mkopo wa gani.

6. Je Laina inamiliki maduka yake?

Hapana, Laina haina maduka yake yenyewe lakini inashirikiana na wasambazaji katika mikoa mbalimbali katika kuhakikisha wateja wanapata bidhaa zenye ubora.

7. Maduka haya yanapatikana wapi?

Ili kuweza kutambua maduka yetu yalipo tafadhari pakua Application ya Laina au tembelea kurasa zetu za mtandaoni au namba ya msaada kwa mteja.

Application : Google store -> Laina Finance

Website :  www.lainafinance.com/sw/maduka-yanapopatikana

Support Number : 0746 821 402

8. Je Nawezaje kuona maduka yalipo?

Ni rahisi, katika application yetu ya kwenye simu au kwenye kurasa zetu za mtandaoni

9. Vifaa mnavyokopesha vina ghalama ya kiasi gani?

Tunatoa mkopo wa kuanzia kifaa cha kiasi cha chini kabisa 50,000 mpaka 3,000,000 kwa kutegemea taarifa za mikopo ya mteja.

10. Je ntapata risiti ya manunuzi?

Ndio ni haki yako kama mteja kupata risiti ya malipo kabla ya kutoka dukani.

11. Naweza ongezea pesa taslimu kwenye kiwango nilichofanikiwa kukopesha?

Ndio, kiasi kilichoongezwa kitalibwa moja kwa moja kwa muuzaji katika duka.

12. Ukinunua kifaa,Ni makubaliano na nani?

Haya ni makubaliano ya mteja na Laina.

13. Kuna malipo ya namna gani?

Malipo yanapishana kutokea kiasi cha chini 20%-40% ya malipo ya awali ya thamani ya kifaa kwa muda wa miezi 3,6 hadi 12.

14. Ni nini matokeo ya kutokulipa?

Adhabu ya penati 10% kwa wiki ambayo hujikusanya kutokea kwenye marejesho ambayo hayajakamilishwa mpaka deni kamili limalizike.

15. Ni nini kitatokea nikihitaji kumaliza deni mapema?

Tunapendekeza malipo kabla ya mwisho wa marejesho sababu hii inakuongezea thamani ya kuaminika na hivyo ni rahisi kupanda kiwango cha mkopo wa kifaa kizuri Zaidi lakini ni rahisi kuaminika na Taasisi zingine na kupata mikopo mbalimbali.

16. Ni lini natakiwa kuanza kufanya marejesho ya kwanza?

Marejesho ya kwanza ni siku 30 tokea siku uliyolipa malipo yako ya awali ya kifaa ulichokopeshwa.

17. Ni vipi na ni wapi natakiwa kufanya malipo yangu ya awamu?

Malipo yako yote waweza kuyafanya kupitia Application ya Laina kwenye simu yako

18. Naweza kulipa kupitia mitandao ya simu?

Ndio, Unaweza kulipia marejesho kupitia aina yeyote ya mtandao wa simu kama Airtel,  Vodacom,   Tigo,  Zantel

19. Itakuwaje nikihitaji kifaa kingine?

Utaweza kupata mkopo wa kifaa kingine baada ya kukamilisha malipo ya mkopo wa kwanza.

20. Nini faida ya kuwahi kumaliza deni?

Rekodi nzuri ya mkopo inakuongezea uaminifu wa kupewa mkopo mkubwa zaidi  na rekodi nzuri ya kukopa kwenye tasisi zingine.

21. Nani atahusika kama kifaa(simu) isipofanya kazi?

Muuzaji atahusika na tunatoa mikopo kwa vifaa vyenye kinga ya uangalizi kwa muda usiopungua mwaka mmoja.

22. Je, ntaendelea kulipia simu kama imeibiwa?

Ndio, na unashauriwa kutunza kwa umakini kifaa ulichokopeshwa na kukamilisha mkopo wako.

23. Nini kitatokea nikiamua kukimbia na kifaa bila kukamilisha malipo?

Taarifa zako zitafikishwa kwenye bodi ya wakaguzi na wasimamizi wa mikopo pamoja na benki kuu ya Tanzania ambayo itaharibu rekodi yako yote ya mikopo na hivyo hutoweza kukopa benki yeyote au kwenye mtandao wowote wa simu ya mkononi.

24. Je, mna namba ya msaada?

Ndio, namba ya msaada kwa mteja ni 0746 821 402 au tuma barua pepe kupitia anuani info@lainafinance.com

Uliza swali